Thursday, February 9, 2017

RASHID MATUMLA ASIMULIA KIPIGO CHA MWANAYE KUTOKA KWA ASKARI MAGEREZA


Rashid (kulia) na Mohammed Matumla wakiwa mazoezini.

Bondia Rashid Matumla amesimulia na kusema mwanaye Mohammed Matumla ambaye amefanyiwa upasuaji, hakuumia sababu ya ngumi pekee.

Mohammed alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuzichapa na Mfaume Mfaume katika pambano lisilo na ubingwa. Makonde ya Mfaume yalisababisha akimbizwe hospitali na baadaye kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini Matumla amesema, chanzo cha hilo tatizo kwa mwanaye ni kipigo cha askari Magereza.

“Unajua sisi tunaishi karibu na Magereza, askari Magereza waliwahi kumpiga sana Mudy. Walimpiga nusura ya kumuua, hali iliyosababisha tatizo kichwani mwake.

“Daktari katuambia kwamba ngumi ni kama zimetonesha tu tatizo hilo lakini tayari alikuwa nalo.

“Unajua kipindi kile baada ya kupigwa na askari Magereza alianza kuwa kama mwendawazimu hivi. Lakini haikuwa inaonyesha sana.

“Huenda baada ya upasuaji huu, inaweza kusaidia kuliondoa tatizo hili,” alisema Matumla ambaye ni bingwa wa dunia wa zamani, mara tatu.


Matumla amesema mwanaye huyo anaendelea vizuri ingawa daktari ameeleza kutakuwa na tatizo kwake kurejea katika ngumi hasa katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

RAFIKI WA SAMATTA AIVUSHA LEICESTER CITY KOMBE LA FA ENGLAND





Wilfred Ndidi amefunga bao muhimu na kuiwezesha Leicester City kusonga mbele katika raundi ya tano ya Kombe la FA.


Ndidi ni yule mshikaji wa Mbwana Samatta aliyejiunga na Leicester City akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.


Leicester Cuty imeshinda Derby County kwa mabao 3-1 na kujihakikishia kucheza raundi ya tano ya Kombe la FA.


LEICESTER (4-4-1-1): Zieler 6.5; Amartey 7, Benalouane 7, Wasilewski 6.5, Chilwell 7; Albrighton 7, King 7.5, Mendy 6 (Ndidi 91' 7), Gray 8; Kapustka 6 (Mahrez 81'); Musa 6.5 (Slimani 91' 5)
Booked: Mendy, Musa
Manager: Claudio Ranieri 7


DERBY (4-3-3): Mitchell 6; Christie, Keogh 6, Shackell 6.5, Lowe 7; Butterfield 7, De Sart 6, Johnson 6.5 (Vydra 53' 6); Camara 7.5 (Russell 74' 5), Blackman 6 (Nugent 82' 6), Anya 7
Booked: Christie
Manager: Steve McClaren 7
Referee: Mike Jones 4
Man of The Match: Gray
Attendance: 29,648
Player ratings by Laurie Whitwell 













09Feb2017

BREAKING NEWS: MANJI, GWAJIMA WAONDOLEWA SENTRO, HUENDA WAMEPELEKWA KWA MKEMIA MKUU


BAADHI YA WAHUBIRI KUTOKA KATIKA KANISA LA GWAJIMA

Taarifa zinaeleza Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wameondolewa katika kitu Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam.

Mmoja wa mashuhuda amesema Manji na Gwajima wanaweza wakawa wamepelekwa kupimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali au Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Ni kweli hii saa kumi na nusu au zaidi, wameondolewa hapa kituoni. Wawili wamepanda gari aina ya Land Cruiser wakiongozana na askari Polisi kadhaa.


“Gari limeondoka na kuekelea maeneo ya Posta ya zamani. Huu uelekeo huenda kwenye ofisini za mkemia mkuu. Lakini hakuna mwenye taarifa rasmi,” kilieleza chanzo.


Manji na Gwajima walifika kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na suala la madawa ya kulevya baada ya kutuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Yakubu arejea England.


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Everton Yakubu amerudi tena Uingereza.Lakini safari hii Yakubu amerudi akiwa na timu ya daraja la pili iitwayo Coventry City inayoshiriki Ligue One,kocha wa timu hiyo Russell Slade amethibitisha suala hilo.
Yakubu amefunga magoli 96 kati ya mwaka 2013 hadi 2012 na Coventry wameamua kumrudisha ili kujaribu kuinusuru timu yao ambayo hali yake sio nzuri.Kocha wa timu hiyo amesema Yakubu ameanza kufanya nao mazoezi na kama watavutiwa naye atakaa klabuni hapo hadi mwisho wa msimu huu.
Kwa sasa Yakubu ana miaka 34 na alikuwa akicheza soka Uturuki katika klabu ya Kayserispor ambako nako hakuwa akipata namba.Russell anaamini japo Yakubu hakuwa akipata namba huko Uturuki lakini ni mzoefu wa ligi kuu haswa Uingereza,kwani ameshapitia Blackburn,Everton na Portsmouth na hiyo inaweza kuleta chachu katika timu yao kwa sasa.
Inaaminika Yakubu ameonesha uwezo mkubwa mazoezini lakini wanataka kumpa nafasi uwanjani ili kumuona anachofanya katika mashindano “Tuko naye kwa sasa,anafanya mazoezi na sisi,japo umri umeenda lakini rekodi yake ya ufungaji ni muhimu sana kwetu” alisema Russell.

FC Barcelona wanatengeneza rekodi katika kila msimu wa Copa Del Rey. Baada ya kuwaondoa Atletico Madrid katika nusu fainali jana usiku, timu hii sasa imefika hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya 4 mfululizo na mara ya 38 katika historia.


Utawala wa Barca katika Copa del Rey: Enrique na Messi wanaiwinda rekodi iliyodumu miaka 64

FC Barcelona wanatengeneza rekodi katika kila msimu wa Copa Del Rey. Baada ya kuwaondoa Atletico Madrid katika nusu fainali jana usiku, timu hii sasa imefika hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya 4 mfululizo na mara ya 38 katika historia.
Luis Enrique sasa amefanikiwa kuiingiza Barca mara 3 katika misimu yake mitatu aliyokaa Camp Nou – rekodi ambayo Fernando Daucik pekee ndio alifanikiwa kabla na kikosi cha Barca kutoka 1951 mpaka 1953. Kocha huyu Mslovenia, akiwa na timu iliyoongozwa na nahodha Kubala, alishinda makombe yote matatu katika fainali za Copa Del Rey na sasa miaka 64 baadae Luis Enrique ana nafasi ya kuifikia rekodi hiyo ya vikombe hivyo na timu inayoongozwa na LaPurga Messi.
Barca wamefikia hatua hii ya fainali mara 7 katika misimu 9 iliyopita na ndio timu iliyoshinda kikombe hiki mara nyingi zaidi katika historia – mara 28. 
Pep Guardiola alifika fainali ya Copa mara 3 na kushinda mara mbili, wakati Tata Martino alifika mara 1.
Barcelona sasa anamsubiri mshindi wa nusu fainali ya leo kati ya Alaves vs Celta Vigo ili kucheza nae fainali ya michuano hii. 

Simba yamzuia Ndemla kwenda Sweden


Klabu ya Simba imemzuia kiungo wao Said Ndemla kwenda kufanya majaribio kwenye klabu moja ya nchini Sweden iliyomuhitaji Ndemla kwa ajili ya kumfanyia majaribio.
Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amefafanua kwa nini Simba hawajamruhusu Ndemla kwenda nchini Sweden kufanya majaribio kwenye klabu inayomuhitaji.
“Sasa hivi Simba ipo kwenye mapambano ya ubingwa, kulingana na mahitaji Ndemla ni machezaji ambaye mwalimu atamuhitaji zaidi. Ukiangalia katika wiki mbili zilizopita ameweza kucheza karibu muda wote kwa maana hiyo kwa sasa hatupo kwenye kipindi cha usajili kwa hiyo endapo ataondoka kwa sasa hatuwezi kupata mbadala.”
“Mwalimu ameona ni jambo jema kama ataendelea kucheza na kama kutatokea mahitaji yoyote basi klabu itaweza kufanya mazungumzo ya awali na timu husika ili baada ya ligi kuisha aweze kuruhusiwa kwenda kufanya majaribio hayo.”
“Au kama kutakuwa na lolote hapa katikati kutoka kwenye benchi la ufundi basi tutaweza kufanya hivyo.”
Said Ndemla ni miongoni mwa wachezaji walioonesha uwezo mkubwa kwenye game ya Majimaji 0-3 Simba na kufanikiwa kufunga goli moja katika mchezo huo. Tangu kuanza kwa msimu huu, Ndemla amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara nyingi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Sunday, February 5, 2017

UNITED KUFANYA MAAJABU MENGINE YA USAJILI

united wanataka kufanya usajili mkubwa mwingine katika dirisha kubwa lijalo la usajili.Na sasa baada ya Paul Pogna timu ya United inahusishwa na kutaka kumchukua Mfaransa mwingine Antoine Griezman toka Athletico Madrid.
Lakini safari hii United wanataka kuuza baadhi ya majina makubwa ili kuweza kumnunua Griezman.Taarifa zinasema Manchester United watauza wachezaji wakubwa watatu ili kupata pesa za kuweza kumleta Griezman ambae thamani yake ni kubwa.
Tetesi zinasema Griezman ameshakubaliana na Man United kuhamia klabuni hapo kwa dau la £ 100m,huku akiingiza £15m kila mwaka katika mkataba huo.Pesa hizo zinaonekana nyingi sana na ili kujaribu kuweka sawa masuala ya malipo ni lazima baadhi ya wachezaji wakubwa wa United wapunguzwe ili kumpisha Griezman.

Inafahamika kwa sasa Athony Martial hayupo katika uhusiano mzuri na kocha Mourinho.Wakala wa Martial alishajaribu kumuuza mteja wake katika ligi ya Hispania japo jambo hilo halijawezekana lakini inaonekana wazi kwamba Martial anaweza kuwa mmoja ya wanaoondoka.Lakini pia Marouane Fellaini pamoja na kupewa nafasi na Mourinho bado hayupo katika kiwango kizuri na yeye anaweza kumfuata Martial.

United tangu kuondoka kwa kocha Alex Ferguson wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa katika usajili.Tangu Ferguson aondoke Man United wametumia £ 513 katila usajili kiasi ambacho ni kikubwa kuliko kiasi walichotumia Real Madrid na Barcelona katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mchezaji wa tatu ambae inasemekana anaweza kumpisha Griezman ni kapteni Wayne Rooney.Siku za karibuni Rooney amekuwa mchezaji wa akiba lakini pesa ndefu kutoka China zinaweza kuishawishi Manchester United kumuacha aende.Si hivyo tu lakini Rooney mshahara wake mrefu wa £ 300000 kila wiki inaweza kuwa sababu ya United kumpunguza Rooney ambae hata hivyo umri wake umeenda.

United wanapambana sana kurudisha ufalme wao uliopotea kwa muda sasa.Wanajaribu kusajili majina makubwa kwa pesa kubwa na katika kipindi hiki ambacho wachezaji wao muhimu wanaonekana umri kwenda,Griezman anaweza kuwa muarobaini wa tatizo la Manchester United.

FIFA KUITOA UINGEREZA KOMBE LA DUNIA


Sheria za chama cha soka duniani FIFA zinakataza Serikali kuingilia masuala ya soka na adhabu kali hutolewa kwa mwanachama yeyote anayekiuka jambo hilo.Bunge la Uingereza linataka kupiga kura ya kutokuwa na imani na chama cha soka cha nchini humo FA.
Sasa hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo kwani jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia.Endapo bunge litapiga kura hiyo wiki ijayo itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018.
Kesi hii ya Uingereza haina utofauti saana na kesi iliyokuwa ikiwakabili Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kombe la dunia Fifa waliamua kuwatoa Kuwait katika mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.
Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia kwani wanaongoza kundi lao la F.Uingereza wamebakiza mechi 6 tu kufuzu kombe la dunia lakini sheria za Fifa zinaweza kuwazuia kufuzu ama kuendelea na mechi zao kwa sasa.
Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na Fa unakuja baada ya baadhi ya viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao kuhusu FA.

LIPULI FC YAREJEA LIGI KUU BARA




LIPUL FC ya mkoani Iringa imerejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polis Dar na kufikisha alama 29 ambazo haziwezi lufikiwa na timu yeyote kwenye kundi lao la ligi Daraja la Kwanza.
Klabu hiyo kongwe ambayo inanolewa na kocha Richard Amatri, ilianza safari yake vizuri yenye matumaini kurejea Ligi Kuu Tanzania  Bara msimu ujao kwa kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza katika Kundi A.
Akizungumza  kocha wa lipuli Richard Amatri amesema mia yao ilikuwa nikurejea ligi kuu nakufanya mapindunzi ya soka katika mkoa wao wa Iringa, hivyo wanajipanga ili wasishuke daraja tena.
“Mashabiki wetu waendelee kutusapoti na kamwe hatuwezi kuwaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu ili kuwapa matokeo mazuri kama tulivyokuwa tunafanya huku katika ligi daraja la Kwanza”, alisema Amtri.
Aidha kocha huyo amewapongeza viongozi wa Lipuli na wachezaji kwa juhudi walizozionesha kuanzia mwanzo msimu mpaka leo huku wakijivunia umoja waliokuwa nao katika timu yao ndiyo umezaa matunda.
Lipuli inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 29  huku ikibakiwa na michezo miwili mikononi mwao.

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif