Thursday, February 9, 2017

Yakubu arejea England.


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Everton Yakubu amerudi tena Uingereza.Lakini safari hii Yakubu amerudi akiwa na timu ya daraja la pili iitwayo Coventry City inayoshiriki Ligue One,kocha wa timu hiyo Russell Slade amethibitisha suala hilo.
Yakubu amefunga magoli 96 kati ya mwaka 2013 hadi 2012 na Coventry wameamua kumrudisha ili kujaribu kuinusuru timu yao ambayo hali yake sio nzuri.Kocha wa timu hiyo amesema Yakubu ameanza kufanya nao mazoezi na kama watavutiwa naye atakaa klabuni hapo hadi mwisho wa msimu huu.
Kwa sasa Yakubu ana miaka 34 na alikuwa akicheza soka Uturuki katika klabu ya Kayserispor ambako nako hakuwa akipata namba.Russell anaamini japo Yakubu hakuwa akipata namba huko Uturuki lakini ni mzoefu wa ligi kuu haswa Uingereza,kwani ameshapitia Blackburn,Everton na Portsmouth na hiyo inaweza kuleta chachu katika timu yao kwa sasa.
Inaaminika Yakubu ameonesha uwezo mkubwa mazoezini lakini wanataka kumpa nafasi uwanjani ili kumuona anachofanya katika mashindano “Tuko naye kwa sasa,anafanya mazoezi na sisi,japo umri umeenda lakini rekodi yake ya ufungaji ni muhimu sana kwetu” alisema Russell.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif