Thursday, February 9, 2017

RASHID MATUMLA ASIMULIA KIPIGO CHA MWANAYE KUTOKA KWA ASKARI MAGEREZA


Rashid (kulia) na Mohammed Matumla wakiwa mazoezini.

Bondia Rashid Matumla amesimulia na kusema mwanaye Mohammed Matumla ambaye amefanyiwa upasuaji, hakuumia sababu ya ngumi pekee.

Mohammed alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuzichapa na Mfaume Mfaume katika pambano lisilo na ubingwa. Makonde ya Mfaume yalisababisha akimbizwe hospitali na baadaye kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini Matumla amesema, chanzo cha hilo tatizo kwa mwanaye ni kipigo cha askari Magereza.

“Unajua sisi tunaishi karibu na Magereza, askari Magereza waliwahi kumpiga sana Mudy. Walimpiga nusura ya kumuua, hali iliyosababisha tatizo kichwani mwake.

“Daktari katuambia kwamba ngumi ni kama zimetonesha tu tatizo hilo lakini tayari alikuwa nalo.

“Unajua kipindi kile baada ya kupigwa na askari Magereza alianza kuwa kama mwendawazimu hivi. Lakini haikuwa inaonyesha sana.

“Huenda baada ya upasuaji huu, inaweza kusaidia kuliondoa tatizo hili,” alisema Matumla ambaye ni bingwa wa dunia wa zamani, mara tatu.


Matumla amesema mwanaye huyo anaendelea vizuri ingawa daktari ameeleza kutakuwa na tatizo kwake kurejea katika ngumi hasa katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif