Manchester United itamkosa mshambulizi wake nyota, Zlatan Ibrahimovic hadi mwaka 2018.
Zlatan aliumia katika mechi ya Europa baada ya kuruka juu, wakati anatua mguu wake ulipinda kwenda nyuma.
Imeelezwa ameumia misuli mikubwa ambayo imechanika katika goto la mguu wake wa kulia.
Hizi ni habari mbaya kwa mashabiki wote
wa Man United kumkosa mkongwe huyo kwa kuwa katika msimu wa kwanza tu
alishafunga mabao 28.
Siku yake ya kutimiza miaka 36, mwezi Oktoba, mwaka huu itamkuta Zlatan akiwa na nje.
Mechi - 46
Mabao - 28
Assisti - 9
Nafasi alizotengeneza - 88
No comments:
Post a Comment