Mshambuliaji mkongwe, Didier Drogba amepokelewa kwa shangwe wakati akitua nchini Marekani kujiunga na timu ya Phoenix Rising ya mjini Arizona.
Lakini ajabu, mashabiki wengi wa Phoenix walionekana zaidi ni mashabiki wa Chelsea, timu ambayo Drogba alipata umaarufu mkubwa.
Mashabiki hao walitaka Drogba kusaini jezi za Chelsea ya England badana Phoenix ambayo ni timu yao.
Kilichovutia zaidi mashabiki hao walikuwa na jezi mpya zinazotumiwa sasa na Chelsea, zikiwemo zile za nyumbani na ugenini.
Drogba
alipata mafanikio makubwa akiwa Chelsea ambako aliiongoza kubeba
makombe lukuki kama Kombe la Ligi, Kombe la FA, Ubingwa wa England na
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment