Wakati Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za London Marathon, Mtanzania Alphonce Simbu ameshika nafasi ya tano.
Wanjiru aria wa Kenya ameshinda kwa muda
wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na Simbu ametumia saa 2, dakika 9 na
sekunde 9 na kushika nafasi hiyo ya tano.
Inaonyesha anayeshika nafasi ya tano katika mashindano hayo anaibuka na kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).
Hata hivyo, Simbu ambaye alianza vibaya
alilazimika kubadili gia mwishoni na kuwashinda zaidi ya Wakenya sita na
Waethiopia wawili, Mganda mmoja ili kushika nafasi hiyo ya tano.
Nafasi ya pili imekwenda kwa Kenenisa
Bekele wa Ethiopia ambaye mwishoni alichuana vikali na Wanjiru
aliyeonekana kuwa katika kiwango bora.
No comments:
Post a Comment