Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili
ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za
kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini
Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017.
TFF inatambua kuwa
wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu
kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia
kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond
Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa
Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo,
lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi
bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena,
Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia
fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe
michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango
mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama
WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya
mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe
ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi
katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz,
kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787
176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa
makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi
kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia tunaomba
wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo
ya Ijumaa.
No comments:
Post a Comment