Kocha
Mkuu wa Ghana, Avram Grant amesema ni jambo bora na la kujivunia kwa
kikosi chake kufika fainali ya Kombe la Mataifa Afrika na kusema ni raha
isiyo na kifani.
Ghana imetinga fainali baada ya kuwanyoa wenyeji Equatorial Guinea kwa mabao 3-0 katika mechi ya nusu fainali.
Grant amesema kikosi chake chenye wachezaji wengi vijana kimeonyesha kina wale wenye hamu ya kufikia mafanikio.
"Kufikia fainali si jambo lahisi kwa kuwa kuna timu nyingi bora zimeishia njiani.
"Tuko
hapa, sasa ni kujipanga na kuangalia tutafanya nini katika siku ya
fainali," alisema Grant kocha wa zamani wa Chelsea raia wa Israel.
No comments:
Post a Comment