Friday, February 6, 2015
WABUNGE WAVALIA NJUGA TIKETI ZA ELEKTRONIC
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imeitaka serikali kuangalia upya mfumo mzima wa ukataji tiketi wa kielektroniki kwa mashabiki wa mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Imetaka serikali kuitisha kikao cha wadau wote yaani benki ya CRDB,
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), wamiliki wa viwanja, klabu ili kuupitia upya mkataba na kuangalia mfumo mzima wa uendeshaji. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda (CCM), alisema hayo bungeni jana wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka 2014/2015. Alisema kamati hiyo ilifanya ziara katika uwanja huo wa Taifa, Januari 19, mwaka huu na kukagua jinsi mashine za ki- elektroniki katika Uwanja wa Taifa kuona jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi.
Alisema wajumbe walijionea jinsi watazamaji wa mchezo wa mpira wa miguu wanavyoingia kwa njia ya kawaida tofauti na maelezo kuwa wanatumia kadi za mfumo wa kielektroniki. "Aidha, mfumo huo umethibitika kuwa hautumiki na kamati haijaridhishwa na utaratibu wa ukataji tiketi unaotumika sasa na tunaitaka serikali kuitisha kikao cha wadau ili kupitia upya mkataba huo," alisema Mtanda. Alisema kutokana na kamati kutoridhishwa ni vyema kuangalia mfumo huo ili kuongeza mapato kwani bado kuna wanaonunua tiketi hizo kwenye magari na sehemu nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment