Saturday, December 5, 2015

HUYU NDIYE MKALI WA SERIE A


Higuani
Na Simon Chimbo
Magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Gonzalo Higuain dhidi ya Inter Milan katika ligi kuu soka nchini Italia juma hili yalitosha kuipa usukani wa ligi Napoli kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 25, na hayo yote yamewezekana kwa mchango mkubwa wa mshambuliaji Gonzalo Higuain, raia wa Argentina.
Katika mechi iliyokua ya kujua nani ataibuka farasi mshindi katika mbio hizo Napoli kupitia Gonzalo Higuain ilijipatia goli lake la kuongoza katika sekunde ya 65 tu kabla ya kuongeza lingine la pili na la ushindi na kuwaacha vijana wa Roberto Mancini wakitweta katika vita hiyo.
Gonzalo Higuain ameshaweka kambani mara 12 katika michezo 14 ya serie A hadi sasa na kuifanya Napoli kuwa juu ya ligi huku pia wakiwa hawajapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi walipocheza na Sasuollo.
Muargentina huyo anawakilisha vyema falsafa mpya aliyokuja mayo kocha Sarri huku wakicheza mpira wa kasi na kuvutia hususan katika eneo la mwisho la kiwanja, ambapo Higuain amekua akiongoza vyema safu ya ushambuliaji.
Achilia mbali magoli 12 katika michezo 14 lakini pia katoa assists 22 kwa wachezaji wenzake na kuwa na wastani wa asilimia 53 shot accuracy huku Messi akiwa na 59% na Ronaldo 50% ni rekodi adhimu.
Lakini yote haya yamekuja kutokana na ukweli kuwa ujio wa kocha Sarri katika klabu hii umeleta ari na mbinu mpya za ushindi wa Napoli sanjari na fomu ya mshambuliaji Gonzalo Higuain tofauti na kipindi cha kocha Rafael Benitez.
Kocha Rafael Benitez alikua akitumia mfumo wa 4-2-3-1 na kumfanya Higuain awe peke yake muda mwingi mbele na hivyo kushindwa kupata sapoti kubwa ya wenzake, wakati hivi sasa kocha Sarri amekuja na mfumo wa 4-3-3 unaowafanya washambuliaji wa pembeni ya Higuain kushirikiana naye vizuri kutengeneza nafasi za kufunga.
Ujio wa kocha Sarri ni neema kwa Napoli na sasa wanaongoza ligi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25, itakua ni ndoto kwa mashabiki wa Napoli siku wanatwaa ubingwa wa ligi hiyo ‘Scudeto’
Mashabiki wanafurahia soka zuri la kuvutia tofauti na misimu iliyopita, Higuain anafunga magoli, timu inapata ushindi, ni msimu mzuri sana kwa Napoli kama tu wataendelea na kasi hii.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif