Monday, November 14, 2016

Olivier Giroud ana njia mbili za kutoka

Frenchman Olivier Giroud ni chaguo la pili la kocha Arsene Wenger ambae mara nyingi huchagua kumtumia Sanchez kama central striker. Ripoti moya kuelekea January ni kwamba Giroud kama anataka kuwa kwenye kikosi cha kwanza ana option mbili ya kwenda Napoli au Ac Milan.
Giroud ameanza kwenye kikosi cha kwanza mara moja kwenye north london derby lakini mechi nyingine zote ameanzia benchi. Sasa amevunja ukimya na kukubali kwamba huu msimu umeanza vibaya kwake tangu ahamie England mwaka 2012.
Giroud alisema,“Nikikaa kwenye benchi naicheki Arsenal inacheza vizuri bila mimi maana yake treni inaenda vizuri bila mimi. Sasa sitaki iniache mbali sana. Hali ikiendelea hivi itanileta athari hapo baadae, siwezi kucheza mechi moja kati ya tano”.
Pia inasemekana Giroud hakupenda alivyoachwa kwenye kikosi cha mechi ya Champions League kwenye mechi dhidi ya PSG.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif