Monday, November 14, 2016

WAANDISHI WA HABARI UFARANSA WAWAWEKA TRUMP NA ARSENAL DUUUU


screen-shot-2016-11-14-at-10-32-57-am

Vyombo vikubwa vya habari huko Ufaransa vimeingia kwenye aibu ya muda mfupi kwa kuparamia habari ambazo baadae iliwabidi wazitoe kwenye mitandao yao.
Sio Ufaransa peke yake hata mitandao mikubwa duniani walijikuta waki qoute habari hii. Website kama RMC Sport, Yahoo na gazeti kubwa la michezo nchini Ufaransa L’Equipe waliandika kwenye website na kufuta baadae.
Habari yenyewe ni kwamba Donald Trump ni shabiki mkubwa wa Arsenal lakini hapendezwi na mwenendo wa Arsenal kama mashabiki wengine duniani. Source ya kwanza ya story ni mtandao unaitwa Politica ambao walisema kwamba mwanzo mwa mwezi wa tatu walimfanyia interview Trump kuhusu mapenzi yake na michezo.
Politica wakaandika qoute hii ambayo shabiki yoyote wa Arsenal angeisema hivi hivi,“Mimi ni shabiki namba moja wa Arsenal, mimi ni real Gunner na nategemea sisi tuziabishe club nyingine lakini sisi ndio tunaabishwa. Arsene Wenger anaumiza roho za Gunners wengi duniani na mimi ni mmoja wapo.”
“Huyu jamaa anaendesha club kama vile ni mali yake. Sitaki kuona Manchester inatufunga lakini sasa hata Swansea. Arsenal imekua punching bag kwa kila mtu.”
Hii quote ilisambaa sana mara baada ya Trump kushinda urais, lakini hapo nyuma haikusambaa sana kwasababu hakuna aliyeifatilia.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif