Kuna kila ukweli kuwa klabu ya Golden State Warriors inahofiwa kutokana na wachezaji wake nyota ambao wakiwa katika fomu na viwango vyao haishikiki hasa katika ushambuliaji. Alfajiri ya leo almanusura wachezaji wake bora watatu wapate pointi 30 kila mmoja.
Klay Thompson alifunga pointi 30 huku akibadili matokeo katika nusu ya pili ya mchezo huo, Stephen Curry pia alifunga pointi 30 huku akipata mitupo 5 ya pointi 3s, na Warriors wakaichapa Phoenix Suns iliyokuwa imechangamka 133-120.
Kevin Durant aliongeza pointi 29, rebound 9 na assits 5.
Thompson alipata mitupo 11 kati ya 18 huku pia akipata mitupo 5 ya pointi 3 huku pointi 14 kati ya hizo zikiwa kazifunga katika robo ya 4, huku Draymond Green akimaliza mchhezo na pointi 14, assist 11na rebounds 7.
Eric Bledsoe pamoja na T.J. Warren walifunga pointi 20 kila mmoja kwa upade wa Suns.
No comments:
Post a Comment