Nyota
mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Samuel Afful,
ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto kuelekea michuano
mbalimbali itakayoshiriki kuanzia mwezi ujao kutokana na ujio wake na
aina ya wachezaji aliowaona ndani ya timu hiyo.
Mshambuliaji
huyo kutoka Ghana amesaini mkataba wa miaka mitatu juzi akitokea timu
ya Sekondi Hasaacas ya huko, anaungana na nyota wengine Waghana
waliosajiliwa na Azam FC msimu huu, beki wa kati Daniel Amoah, winga
Daniel Atta Agyei na mshambuliaji Yahaya Mohammed.
Afful,
20, alifunga bonge la bao kwa shuti kali kwenye mechi yake ya mwisho ya
majaribio dhidi ya Ruvu Shooting Jumatatu iliyopita katika ushindi wa
3-1 wa Azam FC.
Afful
amesema kwa aina ya wachezaji ambao Azam FC imewasajili kutoka Ghana
akiwemo yeye basi itarajia kuwa na safu tishio ya ushambuliaji kwenye
mechi zinazokuja.
“Nimefurahi
sana kujiunga na Azam FC kama mchezaji mwingine anavyofurahia kusaini
mkataba na timu mpya, namshukuru Mungu kwani yeye ndiye amefanikisha
hili, nimejiandaa vilivyo kuisaidia timu hii na naamini kwa namna
nilivyowaona wachezaji kwenye mechi mbili nilizocheza na usajili
uliofanywa Azam FCitakuwa moto sana kwa mechi zinazokuja na eneo la
ushambuliaji litakuwa tishio,” alisema.
Afful
aliongeza kuwa: “Ni wapya kwenye timu lakini tutakapokuwa tukicheza
wote tutakuwa tukizungumza lugha moja ya kusaidia timu kwenda mbele,
naamini kwa aina ya wachezaji niliowaona na sisi tulioongezeka, Azam FC
itakuwa na kikosi bora kabisa cha muhimu ni mashabiki kujitokeza kwa
wingi kutusapoti, nilifurahishwa na ujio wao kwenye mechi ile iliyopita
(Ruvu Shooting), hali hiyo inatupa nguvu sisi wachezaji.”
Alisema
kuwa Azam FC imesajili watu sahihi kwa ajili ya kuimarisha kikosi huku
akidai kuwa imebakia kwa upande wao kulipa fadhila kwa kufanya vema
uwanjani.
Kinda
huyo wa timu za Taifa za Ghana chini ya umri wa miaka 20 na 23, aliwahi
kuchaguliwa kuwa mchezaji bora anayechipukia kutoka Ghana mwaka juzi,
na anakuja Azam FC akiwa ametoka kufunga jumla ya mabao tisa kwenye Ligi
Kuu ya Ghana msimu uliopita akiwa na Sekondi Hasaacas, Pia alichaguliwa
kuwa mchezaji bora wa Ghana anayechipukia mwaka juzi
Mbali
na kuwepo timu hizo za vijana, atakumbukwa kwa rekodi aliyoweka mwaka
jana ya kuifungia bao muhimu timu ya Taifa ya Ghana chini ya umri wa
miaka 20 (U-20) ilipokuwa ikicheza na Zambia, kwenye ushindi wa mabao
2-1 na kuipa nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini New
Zealand, baada ya kutinga nusu fainali ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana
(U-20) zilizofanyika Senegal mwaka huo.
Afful
pia amewahi kuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana cha
wachezaji wa ndani, kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa
Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika Ghana mwaka juzi na timu hiyo
kushika nafasi ya pili akiwa sambamba na nyota mwingine aliyesajiliwa na
Azam FC, Yahaya Mohamed.
Kikosi
cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki mbili hadi Desemba 3
mwaka huu, kitakapoanza mazoezi ya kwanza kujiandaa na mzunguko wa pili
wa ligi pamoja na michuano mingine mbalimbali.
No comments:
Post a Comment