Msimu uliopita Man United ilisaini deal la miaka 10 na kampuni ya michezo ya Adidas ya Ujerumani.
Udhamini ambao unatajwa kuwa na thamani ya pound milioni 750. Man United ilithibisha kwamba, malipo ya mwaka yatapunguzwa kwa asilimia 30 (zaidi ya pound milioni 20) endapo hawatamaliza katika nafasi zitakazowapa nafasi ya kushiriki michuano ya Champions League kwa mara ya pili mfululizo.
Kikosi cha Jose Mourinho kwa sasa kipo nafasi ya sita kwenye Premier League, pointi nne nyuma kutoka timu za top four.
Kuna kipengele kwenye mkataba wa Adidas kinachoelekeza kwamba, endapo tutamaliza kwenye nafasi zitakazotufanya tuwe nje ya Champions League kwa miaka miwili mfululizo tutakosa kiasi cha fedha kutoka kwenye udhamini,”
Baty pia amesema, Man United itapoteza kitita cha mamilioni kutoka Adidas kama watashindwa kufika hatua inayofuata ya michuano ya Europa League ya msimu huu.
Man United wapo nafasi ya tatu kwenye Kundi A, pointi moja kutoka kwa vinara wa kundi hilo huku zikiwa zimesalia mechi mbili kuhitimisha hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment