DIRISHA
dogo la usajili limeshafunguliwa na sasa gumzo limeanza kila upande
ukiamini fulani anatua timu fulani au anaondoka sehemu fulani.
Hiki ndiyo kipindi kila mtu ana uwezo wa kueleza jambo lake analolijua yeye kulingana na tetesi au hali halisi.
Moja
ya mazungumzo ni kurejea kwa mshambuliaji Emmanuel Okwi, ambaye
inaelezwa anatakiwa kujiunga na Simba akitokea Denmark ambako aliuzwa na
Simba katika klabu hiyo ya SonderjysjkE.
Hanspope amesema haya akihojiwa na radio mojawapo jijini dare es ssalaam
Hans Poppe: Nimesikia
sana mtandaoni, waandishi wakaanza kunipigia na mimi nikaamua
kuzungumza na wenzangu kupata uhakika. Kila mmoja hakuwa akilijua hili.
Sitaki kuzika kichwa changu kwenye mchanga, yaani nifiche au niseme tu.
Nafikiri Okwi hadi sasa hayuko kwenye mipango yetu.
No comments:
Post a Comment