Friday, November 18, 2016

YALIYOJITOKEZA BAADA YA KIJANA CHRISTOPHER KUSIMAMISHWA NA TFF

Mapya yaibuka kuhusu kijana aliyesimamishwa na TFF kwa tuhuma za kusaini timu zaidi ya moja

christopher-mshanga-1

SIKU chache baada ya Shirikisho la soka nchini-TFF kumsimamisha mchezaji, Christopher Paschal Mshanga aliyeichezea Kagera Sugar U20 vs Yanga SC katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya vijana kwa madai ya kusaini timu mbili tofauti (Kagera na Panone FC ya ligi daraja la kwanza).
Uongozi wa Machava FC inayoshiriki ligi daraja la pili umejitokeza na kusema kuwa kijana huyo ni mchezaji wao halali tangu angali na miaka 7 na Panone walimsaini kutoka Machava kwa mkataba wa mkopo wa miezi mitatu.
“Christopher Paschal Mshanga aliyeichezea Kagera Sugar na kusimamishwa kwenye ligi kuu ya vijana U20 si mchezaji wa Panone FC kama inavyosemwa, ni mchezaji halali wa Machava FC ya hapa Moshi. Kila kitu kuhusu yeye kipo Machava, mpaka mkataba aliotolewa kwa mkopo wa miezi mitatu kwenda Panone upo Machava.“
“Mkataba ulipomalizika akarudi katika timu yake, sasa hawa Panone wanasemaje ni mchezaji wao wakati hawakufuata utaratibu wa makubaliano ya kumchukua jumla Paschal?” anahoji kiongozi wa Machava FC mapema leo Ijumaa alipowasiliana na mtandao huu.
“Panone walishindwa kumlipa stahiki zake kama walivyokubaliana na mtu aliyetoa taarifa za kulalamika kuhusu mchezaji huyo si kiongozi wa Panone, lakini cha kusikitisha aliweza kutoa hadi kitambulisho cha mchezaji huyo na kusambaza katika magroup na mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile yeye ni msemaji wa klabu au TFF wakati ni makosa na amefanya vile kwa lengo la kumdhalilisha kijana na kutaka kuharibu kipaji chake.”

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif