BEKI wa kulia wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya, amemtabiria mambo makubwa Mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ambae kwa sasa yupo kwenye kiwango kizuri.
Mbaraka amefikisha mabao 11 tangu asajiliwe na Kagera Sugar akitokea Simba mara baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka moja aliosaini akiwa na timu ya vijana ya Simba.
Shaffihdauda.co.tz. ilizungumza na Kimenya ambaye alisema, kama Mbaraka akiendelea kujituma na kupambana kama ilivyo sasa atafika mbali ila kikubwa asilewe sifa na kusahau majukumu yake ya uwanjani.
“Mimi natamani na ninamuombea katika
kinyanganyiro cha mfungaji bora apate Mbaraka kwani kijana anajua kucheka na nyavu na pia atakuwa amewakumbusha watu kuwa sio timu kubwa tu zinaweza kutoa mchezaji bora hata huku chini zipo,” alisema Kimenya.
Kimenya amenijuza kuwa kuna takriba timu tatu za ligi zinataka saini yake lakini kwa sasa ni mapema sana kuziweka wazi ikiwa bado masuala mengi hayajakamilika .
Beki huyo ambae alikuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Simba msimu huu, lakini viongozi wa Simba walishindwana bei aliyokuwa anataka Kimenya ambayo ilikuwa ni shilingi milioni 40za Tanzania.
No comments:
Post a Comment