1.Magoli mengi kabla ya miaka 19. Wakati Cristiano Ronaldo anajiunga na Manchester United, kabla hajafikisha miaka 19 alifunga bao moja tuu lakini Lioneil Messi naye kabla kufikisha umri huo alifunga mbao 7, lakini hadi sasa Kylian Mbappe kabla siku ya kutimiza miaka 19 haijafika ameshaweka kambani mabao 13 ikiwa ni zaidi ya Ronaldo na Messi ukiyaweka kwa pamoja wakati wakiwa na umri huo.
- Aweka historia UEFA. Bao alilofunga dhidi ya Dortmund lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mfululizo katika michezo yake minne ya mwanzo katika hatua ya mtoano ya UEFA, sio Messi wala sio Ronaldo aliyewahi kufanya jambo kama hilo.
- Historia nyingine Uefa. Ni wachezaji 6 tu ndio ambao wamewahi kufunga katika mechi zao nne za mwanzo walizoanzishwa katika UEFA, katika orodha hiyo Messi na Ronaldo hawapo ila jina la Kyllian Mbappe lipoo.
5.Kushoto na kulia yeye sawa tu. Wakati Messi na Ronaldo wana miguu yao ya mauaji, Kylian Mbappe katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga kwa miguu yoteyote katika champions league.
No comments:
Post a Comment