Friday, April 21, 2017

Ugo Ehiogo afariki dunia, ni nani huyu?

Pengine leo kila mahala unaposoma vyombo vya habari vya kimataifa utakutana na jina la Ugo Ehiogo ambaye amekufa kutokana na shambulio la moyo lililomkuta akiwa kazini na kikosi cha Tottenhma Hotspur chini ya miaka 23.
Ehiogo ana jina la Kinigeria lakini ni mzaliwa wa nchini Uingereza mwaka 1972, alifanikiwa kucheza kwa mafanikio makubwa kama mlinzi wa kati katika vilabu vya Leeds, Aston Villa, Rangers na Sheffield United na timu ya taifa ya Uingereza.
Baada ya kumaliza kucheza soka Ehiogo aliamua kuwa mwalimu wa mpira wa miguu na timu yake ya kwanza kufundisha ilikuwa ni Tottenham Hotspur chini ya miaka 23 na hata shambulio lake la moyo lilimpata asubuhi ya Alhamisi akiwa mazoezini na timu yake.
Siku ya Alhamisi Ehiogo alianguka ghafla mazoezini hapo na kukimbizwa hospitali ambapo taarifa zinasema asubuhi ya Ijumaa alifariki na ameacha mjane aitwaye Gemma na pia mtoto mmoja wa kiume.
Ehiogo ameshawahi kushinda kombe la ligi mwaka 1994 na 1996 akiwa na Aston Villa lakini pia akashinda kombe hilo mwaka 2004 akiwa na Middlesbrough, beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amesema hadi sasa haamini kama Ehiogo ameondoka.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif