Pione Sisto alikuwa wa kwanza kuchungulia nyavu za Genk dakika ya 63 kabla ya Leandro Trossard kuwasawazishia Genk na mchezo kumalizika kwa sare.
Kabla ya mchezo huo Celta Vigo hawajawahi kufungwa na timu yoyote kutoka Ubelgiji na matokeo hayo yaliifanya Genk kutolewa kwa jumla ya mabao 3 kwa 4, kwani mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 3 kwa 2.
Katika michezo mingine iliyopigwa jana ililazimika kuongezwa muda wa ziada ili kumtafuta mshindi wa michezo hiyo, Manchester United na Anderchelt walimaliza dakika 90 kwa sare ya moja kwa moja.
Baada ya dakika hizo 90 kuisha muamuzi aliongeza dakika 30, dakika ya 107 ya mchezo huo goli la Rashford liliivusha Manchester United katika hatua ya nusu fainali ya Europa Champions msimu huu.
Ajax nao bao la dakika ya 120 la Amin Younes lilishuhudia klabu hiyo ikifudhu hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza mchezo huo kwa bao 3 kwa 2 dhidi ya Shalke 04 na mchezo huo kuisha kwa aggregate ya bao 3 kwa 4na kufudhu tena nusu fainali tangia mwaka 1997.
Besitikas na Lyon hadi dakika 120 zinaisha mshindi alishindwa kupatikana japo Bestikas walikuwa wakuongoza 2 kwa 1 lakini aggregate ilikuwa 3 kwa 3 hivyo mchezo huo ilibidi uamuliwe kwa tuta.
Katika hatua ya matuta Lyon ambao walikuwa wageni katika mchezo huo waliibuka kidedea kwa kushinda jumla ya matuta 7 kwa 6 na hivyo nao kuungana na Celta Vigo,Manchester United na Ajax katika michuano hiyo ya Europa.
No comments:
Post a Comment