Mabosi
wa Simba kiroho safi walikubaliana kumsajili beki wa kati wa Prisons,
Nurdin Chona, lakini beki huyo akataka asajiliwe kwa dau la Sh milioni
40, Simba ikanywea, ikatulia.
Kwa
kuwa Simba wana shida, wakambembeleza Chona awashushie bei, lakini beki
huyo akaendelea kubaki palepale kwamba anataka Sh milioni 40. Simba
ikaona isiwe shida ikaachana naye.
Hesabu
za Simba zilikuwa ni kumsajili Chona ili kuimarisha safu yake ya beki
ya kati ili aweze kushirikiana na Novatus Lufunga na Juuko Murshid.
Baada
ya kuona mambo yanashindikana, Simba ikazungumza na beki wa Mwadui FC,
Emmanuel Semwanza ambaye alikubali kusaini kwa Sh milioni 20 tu kwa
mkataba wa miaka miwili. Mambo yakaishia hapo.
Hebu
sikia kilichotokea baada ya Semwanza kusajiliwa, mmoja wa mabosi wa
Simba alisema: “Aliposikia tumemsajili Semwanza, eti Chona akatuomba
tumsajili hata kwa Sh milioni 20.
“Tukamjibu
palepale kwamba, basi haitawezekana maana tumeshampata mbadala wake na
mambo yakaishia hapo, kilichomponza ni tamaa tu,” alisema bosi huyo.
Licha ya Chona, Simba bado inahusishwa na taarifa za kumnyakua Salum Kimenya wa Prisons.
Alipotafutwa
Chona alisema: “Ni kweli Simba tuliongea lakini hatukifikia mwisho,
tulipishana kwenye kipengele cha maslahi lakini pia ishu ya mkataba
wangu na Prisons ilichangia. Nina mkataba mrefu wa miaka minne, hivyo
kwa kiasi kikubwa nao ulichangia tusifikie mwisho wa mazungumzo yetu.”
No comments:
Post a Comment