CHIRWA NA NGOMA WAKISHEREKEA BAO WAKATI WAKIWA FC PLATINUMS YA ZIMBABWE |
Kiroho
safi straika Donald Ngoma ameelezwa kupendekeza usajili wa straika
Obrey Chirwa katika klabu yake ya Yanga akimtosa Walter Musona aliyekuwa
chaguo lingine la timu hiyo.
Yanga
ilikuwa na mpango wa kusajili straika mwingine wa kigeni baada ya
kutoridhishwa na uwezo wa Issouf Boubacar raia wa Niger, hivyo ikawa na
chaguo la kwanza Danny Phiri ‘Deco’ wa Chicken Inn ya Zimbabwe.
CHIRWA WAKATI AKITUA DAR, JANA. |
Chaguo la pili la Yanga lilikuwa Chirwa wa FC Platinum pia ya Zimbabwe na la tatu lilikuwa ni Walter Musona pia wa Platinum.
Bosi
mmoja wa Yanga anayeshughulikia mambo ya usajili aliliambia Championi
Jumamosi kuwa, baada ya kushindwa kumsajili Deco, Ngoma aliwashauri
kuhakikisha anasajiliwa Chirwa badala ya Musona.
“Ni
jambo la ajabu kabisa kwani Ngoma alitueleza kuwa ni bora tumsajili
Chirwa ambaye ni raia wa Zambia kuliko Musona ambaye ni Mzimbabwe
mwenzake.
“Tulishangaa
kwani tulidhani labda angempendekeza raia mwenzake wa Zimbabwe, (Ngoma)
alitueleza Chirwa ni mzuri zaidi ya Musona, na sisi tukafuata ushauri
wake,” alisema bosi huyo.
Chirwa
aliwasili nchini jana jioni na alikuwa na mazungumzo ya mwisho na
uongozi wa Yanga jioni hiyo kabla ya kusajiliwa halafu leo ataenda
Algeria kujiunga na kikosi cha timu hiyo ambacho kesho kinacheza na MO
Bejaia katika Kombe la Shirikisho Afrika.
No comments:
Post a Comment