Timu
hiyo, hadi hivi sasa imesajili wachezaji wanne akiwemo Rasta, Muzamir
Yassin pia kutoka Mtibwa, Jamal Mnyate na Emmanuel Semwanza wote wa
Mwadui FC.
Licha
ya kuwasajili nyota hao, Simba bado inaendelea kufanya mazungumzo ya
usajili na wachezaji wengine akiwemo kiungo wa Mtibwa, Shiza Kichuya.
Kwa mujibu wa taarifa 'Rasta' amesaini mkataba wa miaka miwili jana mchana.
Moja
ya makubaliano ya Rasta na Simba ni kulipwa Sh 250,000 kila Simba
inaposhinda yeye akiwa kikosini lakini dau lake la usajili limefichwa
kwa sababu maalum.
“Tulikuwa
hatutaki kuona masuala yetu ya usajili yanafanyika kwa uwazi, kwa
sababu nusu ya wachezaji tunaowahitaji kwa ajili ya kuwasajili wana
mikataba na timu zao.
“Ukiachana
na Rasta wachezaji wengine ambao tumemalizana nao ni Yassin, Mnyate na
Semwanza. Huyu Rasta kasaini leo (jana) mchana, amesaini mkataba wa
miaka miwili kwa sharti la kulipwa Sh 250,000 kama posho yake kila timu
inaposhinda,” alisema mmoja wa viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba.
Alipotafutwa
meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo kuzungumzia hilo, alikiri
taarifa hizo kuwa za kweli Rasta amesaini mkataba wa miaka miwili Simba.
“Nikutoe
hofu tu, Mohammed (Rasta) amesaini mkataba leo (jana) hii na hapa
ninapoongea na wewe, ndiyo tunamalizana kwa maana ya kusaini mkataba huo
wa miaka miwili,” alisema Kasongo.
No comments:
Post a Comment