Kuna
uwezekano mkubwa beki mpya wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’
akachezeshwa kesho Jumapili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, mwenyewe
amesema akipata nafasi hiyo hatatoka kikosi cha kwanza.
Yanga
kesho Jumapili inatarajiwa kucheza na MO Bejaia mechi ya Kundi A ya
Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa l’Unite Maghrebine uliopo
Bejaia, Algeria.
Dante
aliyesajiliwa na Yanga siku chache zilizopita kutoka Mtibwa Sugar, ana
nafasi kubwa ya kucheza katika beki ya kati na Kelvin Yondani kwani Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hayupo kikosini.
Cannavaro
anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Sagrada
Esperanca na Vincent Bossou ambaye hucheza nafasi hiyo, naye hakufanya
mazoezi kikamilifu na wenzake kutokana na kuchelewa kujiunga nao.
Akizungumza kutoka
Algeria, Dante alisema: “Kwa jinsi nilivyo fiti kutokana na mazoezi
niliyofanya kambini Uturuki, naamini nikipata nafasi kikosi cha kwanza
sitatoka.”
“Nitacheza
kwa juhudi kubwa kumvutia kocha ili awe ananipa nafasi kila mara
kikosini, labda nisipangwe lakini nikicheza tu nitahakikisha sikai
benchi.”
Dante
anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo mkabaji, alisema
kambi ya muda iliyoweka Yanga nchini Uturuki tangu Jumapili iliyopita
hadi jana Ijumaa, imewasaidia kwa kiasi kikubwa.
Mbali
ya Dante, hadi sasa Yanga imewasajili Hassan Kessy kutoka Simba, Juma
Mahadhi (Coastal Union) na Beno Kakolanya kutoka Prisons.
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment