Ili
kuhakikisha inafanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Ndanda FC
imepanga kusajili wachezaji saba kutokana na ripoti ya kocha wao, Malale
Hamsini kutaka wafanye hivyo.
Katibu
Mkuu wa Ndanda, Selemani Kachele alisema, wamepanga kuongeza wachezaji
saba ili kuimarisha kikosi chao kiweze kupambana ipasavyo.
“Kati
ya hao wachezaji saba, mabeki wawili, viungo watatu, straika mmoja na
kipa mmoja, tukifanya hivyo tutakuwa fiti zaidi,” alisema Kachele.
Ndanda haikuwa na msimu mzuri sana katika msimu uliopita, na ililazimika kufanya kazi ya ziada ili kubaki Ligi Kuu Bara.
No comments:
Post a Comment