Kama unakumbuka nilikupa habari ya Carrick kusema kwamba anadhani huu utakua ni msimu wake wa mwisho ndani ya OT. Carrick alisema hayo akielezea pia kuja kwa damu changa kwenye kikosi cha manager Jose Mourihno.
Carrick mwanzoni alisani mkataba wa mwaka mmoja mwezi June ina imeonekana amemfurahisha manager wake kwa muda wote tangu aongeze mkataba huo. Kutokana na kuwa na midfielder kama Ander Herrera na Paul Pobga, waandishi wa habari walimuuliza Jose kama kuna uwezekano wa Carrick kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho,“Msimu mmoja wa ziada anastahili. Siku zote nimempenda sana Carrick. Yeye ana miaka 35 ni habari mbaya sana kujua miaka inaenda sana kati yetu. Lakini Michael ni mchezaji mzuri sana na badala ya kuwa manager wake alivyokua ana miaka 25 nimekua manager wake akiwa na miaka 35.”
Mourinho aliongeza, “Tuna maelewano mazuri na tunajua anaweza kucheza. Najua ni muda gani yupo tayari kucheza na muda gani anahitaji kupumzika. Bado nipo na Carrick labda kwa msimu mmoja tena baada ya huu”
No comments:
Post a Comment