Mapema wiki hii kiungo mshambuliaji wa klabu ya Ac Milan, Suso alitoa ahadi kuwa angetembea kwa mguu kurudi nyumbani iwapo kama angefunga magoli mawili na kuendelea dhidi ya wapinzani wao Inter Milan kwenye Derby maarufu kama della Madonnina, kitu ambacho alifanikiwa kukifanya uwanjani kwa mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mabao mawili ya Suso ni kama yalikuwa yameihakikishia Ac Milan iinayofundishwa na Vincenzo Montella lakini goli la dakika za mwisho la Ivan Perisic lilihitimisha mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kwa sare.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool na mzaliwa wa mji unaoitwa Cadiz nyumbani kwake ni jrani na maeneo ya Milan maarufu kama Milanello, ambao makadirio yake ni kama kilomita 45 mpaka 50 atakazotakiwa kutembea, hivyo ni jukumu analotakiwa kulitimiza.
Sio Masikhara.
No comments:
Post a Comment