Monday, November 21, 2016

Zidane na rekodi bora ya La Liga kuliko Guardiola


Ushindi usio na mashaka katika dimba la Vicente Calderon umemaliza ubishi juu ya uwezo wa mbinu wa kocha Zinedine Zidane, pia ushindi wa jumamosi umemfanya Zizzou kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi baada ya mechi 32.
Cha kushangaza pamoja na kwamba aliweza kushinda Undecima, UEFA Super Cup na kucheza mechi 28 bila kupoteza – mafanikio haya yalionekana hayatoshi, kwa sababu wengi walikuwa wanaamini timu ilikuwa haichezi vyema na ilikuwa inaenda kibahati bahati.
Alikuwa na majeruhi wengi kabla ya Derby, lakini uendeshaji mzuri wa kikosi ulimaanisha hata wachezaji ambao hawakuwa wakipata nafasi ya kucheza, walikuwa na utayari wa kutoa mchango wao kwenye kikosi – hasa Isco.
Zidane pia ameonyesha kuwa mbunifu kimbinu, akitumia mfumo wa 4-2-3-1 Isco akicheza nyuma ya Cristiano Ronaldo – mfumo huu ulitoa matunda mazuri na uliwa-surprise Atletico.
Zidane pia amekuwa akihamia kwenye mfumo wake wa kawaida 4-3-3 na 4-4-2 kulingana na wachezaji alionao, na unyambulifu huu wa mbinu umekuwa mzuri kwenye kikosi chake.
Baada ya mechi 32, Zidane amefanikiwa kupata pointi 83, mbili zaidi ya Pep Guardiola alizofanikiwa kupata wakati akiwa na kikosi bora cha Barcelona.
Ameshinda mechi 26, sare 5 na amepoteza mchezo mmoja tu, na baada ya kukosa ubingwa wa La Liga kwa muda mrefu, hiki ni kipaumbele na Zidane ndio mtu wa kufanikisha.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif