Shirikisho la Soka la Sweden (SvFF) limetangaza kutengenezwa kwa sanamu
maalum la mshambuliaji nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden na nahodha, lakini ni
Mswidi aliyeshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Sweden kwa miaka 10
mfululizo.
Sanamu lake litawekwa nje ya Friends Arena katika jiji la Stockholm.
Hali hiyo ni kuonyesha kuthamini mchango wake akiwa na timu ya taiga ya
Sweden lakini kuwasaidia wanamichezo chipukizi kuhakikisha wakiwa na
hamu ya kupata mafanikio.
Zlatan ambaye sasa ana umri wa miaka 36, akiwa na timu ya taifa ya
Sweden amecheza mechi 114 na kufunga mabao 62. Alitangaza kustaafu baada
ya michuano ya Euro iliyofanyika nchini Ufaransa, hivi karibuni.
TAKWIMU ZAKE
KLABU ALIZOPITIA: Malmo, Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, AC Milan, PSG, Manchester United
MECHI: 646;
MABAO: 381
MECHI TIMU YA TAIFA: 116;
MABAO: 62
MAKOMBE:
2009/10 La Liga, 4x Serie A (Mara tatu akiwa na Inter, Mara moja na AC
Milan), 4x Ligue 1, 2x Eredivisie, 2010 FIFA Club World Cup, 2010 UEFA
Supercup
No comments:
Post a Comment