Uongozi wa Yanga umeapa kutofanya papara katika suala la usajili na badala yake, kila kitu kitakwenda kiufundi.
Habari za ndani kutoka kamati ya mashindano ya Yanga zimeeleza, mambo yamekuwa yakifanyika taratibu na kufuata weledi.
“Hakutakuwa
na chochote cha haraka, kila kitu kitakwenda kwa mpangilio na uongozi
ndiyo unajua kila kitu. Lengo letu ni kufikia malengo.
“Hatuwezi
kuwa na hofu kwa kuwa bado tuna kikosi bora, mabadiliko hayawezi kuwa
makubwa kwa kuwa tunahitaji kuimarisha pekee,” kilieleza chanzo.
Imeelezwa, benchi la ufundi limeendelea kupewa nguvu ya kufanya mabadiliko ili mambo yakae sawa.
Yanga
ndiyo timu inayoongoza kuwa na wachezaji wengi waliokaa pamoja na
imeendelea kutesa kwa kutwaa ubingwa kwa misimu miwili mfululizo.
No comments:
Post a Comment