Samir Nasri na William Gallas waliwahi kucheza wote katika klabu ya Arsenal huku wakiwa wote kwa nyakati kadhaa katika timu ya Taifa, ingawa mahusiano yao yalikuja kuingia doa mwaka 2008 siku ambayo Nasri alikalia kiti/siti ya Thierry Henry kwenye basi la timu.
Mambo yalienda vibaya zaidi pale ambapo Nasri alipotoa shutuma kadhaa dhidi ya beki huyo ambapo hata hivyo Gallas alipinga na sasa ameibuka na tukio la mwaka 2009 ambapo alihisi ameundiwa mbinu za kuteswa na shoti ili apooze kwa muda.
‘Manchotakiwa kufahamu ni kuwa kipindi chote nilikuwa naishi katika hoteli nikiwa na familia yangu,’ alisema Gallas wakati akizungumza na kituo cha Televisheni cha Ufaransa, RMC.
‘Nilikuwa na binamu zangu tukipata chakula, ilikuwa ni katika hafla ambapo tulikuwa tunakutana timu nzima ya Ufaransa.
‘Baada ya chakula nilitoka nje ya hoteli na nikashuhudia watu kadhaa wakija na kutaka kuzungumza nami.
‘Mwanzoni sikutaka, kabla sijamgundua mtu mmoja ambaye mara nyingi alikuwa na Samir kwenye viwanja vya mazoezi vya Arsenal.

‘Siku chache kabla, tulikuwa na mvutano hasa kutokana na tuhuma dhidi yangu ambazo hata hivyo sikuzipenda.
‘Huyu mtu alitaka tuzungumze lakini pia tuonane na Samir, ambaye alikuwa kwenye gari umbali mfupi kutoka nilipokuwa hivyo nikajiandaa kumfuata lakini binamu yangu ambaye ni askari akanieleza kwa lugha yetu kuwa nisimfuate.
‘Wakati huo huo nikirudi ndani nikaona mtu akinyatia ndani ya hotel huku ameshika begi.
‘Kwenye begi lile kulikuwa na vifaa vya shoti. sikujua kwanini.
‘Bahati nzuri nilikuwa na watu siku hiyo hivyo hata sifahamu ni nini kingeweza kutokea.’
Ni Gallas pekee ambaye kasema stori hii ni ya kweli na ilitokea, lakini ni kitu ambacho kiliwaacha mdomo wazi wachambuzi wenzie waliokuwa wote kwenye kituo hicho cha RMC.
Wachezaji wenzie wa zamani Emmanuel Petit na Franck Le Bouef walisikiliza huku wakionekana kushitushwa na anahokisema William Gallas.
Hakuna ushahidi mpaka sasa, zaidi ya maneno ya Gallas, kuwa Nasri alihusika na tukio la kumpigisha shoti mchezaji mwenzie.

No comments:
Post a Comment