Rooney alikuwa moja ya wachezaji walioanzia benchi, huku Mourinho akichagua kuanza na Mata, Anthony Martial na Marcus Rashford kwenye eneo la ushambuliaji.
Nahodha huyo wa England alipita katika wiki ngumu kuelekea mchezo huo uliopigwa Old Trafford, huku kukiwa na picha zilizoenea ambazo alipigwa akiwa amelewa wakati wa wiki ya michezo ya timu za taifa.
Lakini Mourinho amedai kwamba taarifa hizo hakuzitumia kama sababu ya maamuzi yake hayo isipokuwa aliangalia zaidi kasi ya wachezaji uwanjani katika mchezo huo.
“Nilijua tunaenda kucheza kwa kumiliki mpira,” alisema Mourinho na kuongeza. “Arsenal ni timu ambayo huruhusu wapinzani wacheze mpira.
“Nilidhani tungekuwa na wasaa mzuri wa kuchezea mpira na kuleta urahisi kwa washambuliaji wetu.
“Niliamini kwa aina ya wachezaji kama Juan Mata, Anthony Martial na Marcus Rashford wangefaa zaidi kwababu wana kasi zaidi ya Wayne Rooney, wazuri zaidi inapofika wanapambana ana kwa ana na mpinzani. Mimi nilidhani yalikuwa ni maamuzi sahihi kwangu.”
No comments:
Post a Comment