Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba Hector Bellerin
anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nne baada ya kupata majeraha katika mchezo
dhidi ya Tottenham.
Beki huyo wa kulia Mhispania aliumia kifundo cha mguu wakati wa
mchezo dhidi ya Spurs uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kabla ya kupisha
mapumziko ya mechi za kimataifa.Katika mkutano na wanahabari leo Wenger amesema: “Hectoer atakuwa nje kwa wiki nne. Alipata majeraha sekunde kumi tu kabla ya mchezo dhidi ya Spurs kumalizika.”
Kwa hali hiyo Bellerin ataukosa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United unaotarajiwa kufanyika Jumapili ya wikiendi hii katika Uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment