Thursday, November 17, 2016

Tetesi : Theo Walcott anaweza kukosa mechi ya Manchester.

screen-shot-2016-11-17-at-3-44-47-pmUmekua mwanzo mzuri wa msimu kwa Walcott ambae alianza kwa maswali mengi kutoka kwa mashabiki kwa nafasi yake ndani ya club hiyo. Hatimaye aliweza kuwanyamazisha kwa kufanya vizuri baada ya kufunga mara tano katika mechi 11 alizocheza pamoja na kutoa assist tatu.
Hivi sasa wakielekea kwenye mechi dhidi ya Manchester united inasemekana kwamba anaweza kukosa mechi dhidi ya mahasimu wao Manchester united. Sio kwamba ana majeraha hapana,  mke wake Melanie Slade anategemewa kujifungua muda wowote kuanzia sasa hivi.
Mke wake akiwa anajifungua au akijifungua kwa kawaida Theo Walcott atahitajika kuwa karibu na mke wake.Sasa mashabiki wa Arsenal wanatakiwa kusubiri hadi mwisho kuona kwamba shemeji yao atajifungua muda gani ili Walcott awepo kwenye line up

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif