Moja ya habari ya moto kuhusu swala zima la uhamisho ni kuhusu tetesi za Countinho kuhusishwa na ishu ya kutakiwa na Barcelona. Tetesi hizi zimepamba moto baada ya mchezaji wa zamani wa Barca Xavi kusema kwamba playmaker huyo wa Brazil ni moja kati ya wachezaji wachache wanaoweza kuongeza kiwango chao kama akijiunga na Barca.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Klopp alisema hivi kuhusu mchezaji huyo mwenye miaka 24,“Yeye ni mchezaji mzuri sana na siku zote utataka kukaa nae kwa muda mrefu zaidi. Ni swala zima la kutengeneza hali na fikra ya kwamba hakuna mtu yoyote anayetaka kuhama.”
Klopp aliendelea, “Mawazo yangu ni kwamba anajiskia vizuri sana kuwa pale na naamini ana maisha mazuri hapo mbeleni na Liverpool”. Maneno yote haya Kwa uwezo wa kipenda wa club ya Liverpool wanaweza kushinda jaribio lolote la kumchukua mchezaji huyo kama kwa sababu ya pesa.
No comments:
Post a Comment