Thursday, November 17, 2016

Timu za Basketball zilizotwaa ubingwa wa NBA mara nyingi (+Picha)

Nahafahamu upo shabiki wa nguvu wa mpira wa kikapu duniani, na hautapenda kupitwa na hii list iliyozitaja timu 5 za Baskteball kutoka kwenye ligi kuu ya NBA ambazo zimefanikiwa kuchukua ubingwa wa mara nyingi.
Takwimu imezitaja timu zilishoshiriki mashindano ya mpira wa kikapu kuanzia mwaka 1976 ikiwemo club ya San Antonio Spurs ambayo ilianzishwa mwaka 1967 lakini ilijiunga na ligi ya NBA mwaka huo huo 1976.
Zipo pia timu kama Los Angeles Lakers ambayo ilikuwa ikiitwa Minneapolis Lakers kuanzia mwaka 1947 mpaka 1960. Kuna club ambazo zimefanikiwa kutwaa kikombe cha Larry O’Brien NBA Championship ambacho hutolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu kwa mshindi wa fainali za NBA kila msimu.
Kikombe hicho kilikuwa kinaitwa Walter A. Brown mpaka kufikia mwaka 1984 kilipobadilishwa na kuitwa Larry O’Brien NBA Championship.
Nimeziweka hapa timu tano bora zilizochukua ubingwa wa Basketball mara nyingi zaidi.
       Jina la Timu Idadi ya Ubingwa wa NBA  Miaka ya Ushiriki
1.  Boston Celtics
(Boston, Massachusetts)
17 Miaka 70 
(1946 mpaka 2016)
2. Los Angeles/Minneapolis Lakers
(Los Angeles, California)
16 Miaka 69 
(1947 mapaka 2016)
3. Chicago Bulls
(Chicago, Illinois)
6 Miaka 49 
(1966 mpaka 2016)
4. San Antonio Spurs
(San Antonio, Texas)
5 Miaka 40 
(1976 mpaka 2016)
5. Golden State Warriors
(Oakland, California)
4 Miaka 70
(19 mpaka 2016)








No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif