Mtandao wa Millardayo.com umeripoti kuhusu sababu iliyotolewa na mchezaji wa zamani wa Simba Justice Majabvi kuamua kuachana na klabu hiyo ya msimbazi licha ya kufanya vizuri kwenye mechi ligi kuu Tanzania bara na kombe la FA (Azam Sports Federation Cup).
Kiungo huyo raia wa Zimbabwe, alihudumu Simba kwa msimu mmoja na katika msimu huo alicheza kwa asilimia 90 ya mechi zote za Simba na kuonesha kiwango kizuri.
Baadae mwisho wa msimu alivyoenda kwao Zimbabwe hakutaka tena kurudi Simba, millardayo.com imempata akiwa kwao Harare, Zimbabwe na kueleza nini kilimfanya aondoke Simba licha ya kucheza kwa kiwango kizuri.
“Kwanza nilitaka kurudi nyumbani kukaa karibu na familia yangu na kuna vitu baadhi vilikuwa haviendi sawa kati yangu na timu, sasa sikutaka kumsumbua mtu wala ku ‘make stori’ nikaona njia sahihi ni mimi kuondoka tu.”
“Kama wanataka nirudi nilazima wazingatie professionalism unajua mimi ni mchezaji professional sitokei mtaani, katika maisha yangu ya soka sikuwahi kuwa na ugomvi na yeyote katika soka na sipendi migogoro, mimi napenda kucheza soka.”
“Kwa sasa nipo tu, sichezi mashindano yoyote zaidi naenda kucheza timu za malegend pale ninapojisikia haiko serious kihivyo, huwa najumuika na wachezaji wa timu za zamani, bado najihisi naweza kucheza na kufanya vizuri lakini ili nirudi kucheza ni lazima nipate mahali sahihi.”
No comments:
Post a Comment