Thursday, November 17, 2016

Wayne Rooney aomba radhi kwa picha zake kusambaa

screen-shot-2016-11-17-at-6-13-03-pmWayne Roonye ameingia kwenye vichwa vya habari siku hizi mbili zilizopita kutokana na picha zake kusambaa akiwa ameonekana kalewa. Picha hizo zinamuonyesha Rooney akiwa amelewa na mashabiki zilitolewa na mtandao wa The Sun zikiwa na kichwa habari kwamba Rooney alilewa hadi anashindwa kusimama.
Japokua ilikua ni siku off kwa Rooney ambapo anaruhusiwa kuwa kwenye starehe zake kama hivyo lakini bado ammemtumia msemaji wake kuomba msamaha kwa picha kusambaa. Msemaji huyo alisema,“Wayne Rooney anajiskia vibaya kwa picha alizopiga na mashabiki kusambaa. Japokua ilikua ni siku yake ya kupumzika anaamini zile picha sio sawa kusambaa kwa mtu kama yeye.”
Msemaji huyo aliendele,” Leo mapema Rooney aliongea na Gareth Southgate na Dan Ashworth kuhusu hizi picha. Pia Wayne anajiskia vibaya zaidi kwa mashabiki wenye umri mdogo ambao wameona hizi picha.”
screen-shot-2016-11-17-at-6-13-12-pm screen-shot-2016-11-17-at-6-13-27-pm

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif