Thursday, November 17, 2016

Rais wa Barcelona amesema hivi kuhusu tetesi za mkataba wa Messi.

screen-shot-2016-11-17-at-6-00-39-pm
Lionel Messi anamaliza mkataba wake wa sasa ifikapo 30 JUne 2017, kutokana na ripoti za gazeti la Marca mchezaji huyo mwenye miaka 29 anaweza kusepa.
Messi ambaye analipwa pesa nyingi zaidi kwenye listi ya wachezaji wa Barcelona anatarajiwa kuwa mchezaji ghali zaidi duniani akisaini mkataba mpya.
Kutokana na Alves kuondoka Barcelona waandishi wengi waliandika kwamba kitendo hicho hakikumfurahisha Messi. Kuchelewa kuasaini mktaba mpya wakati wa sasa hivi umebaki chini ya mwaka mmoja vinaleta viashiria vibaya kwamba huenda Messi akasepa.
Wakati wa sherehe ya kutangaza sponsor mpya wa jezi za Barcelona rais wa club hiyo alisema,“Sisi tunashawishika kwamba Messi atamaliza maisha yake ya soka hapa Barcelona. Yeye ni mchezaji aliyetuongoza kwenda kwenye mafanikio ndani ya miaka yote hii”.
Kwa ujumla Messi alecheza mechi 548 akifunga mara 472 na kutoa assist mara 219. Bado kubaki kwake ni kitendawili na kama akiondoka ataenda wapi?. Endelea kufatilia shaffihdauda.co.tz kwa ajili ya updates

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif