Thursday, November 17, 2016

Warriors waharibu Usiku wa Drake…

k
Klabu ya Golden State Warriors haikujali kama Toronto Raptors waliuandaa usiku wa kuamkia leo kuwa usiku wa Drake. Walimaliza kazi waliyotakiwa kuifanya.
Ikumbukwe kuwa rapa huyu raia wa Canada ambaye pia ni balozi wa klabu ya Toronto Raptors kote duniani hakuwahi kushuhudia klabu yake hiyo ikipoteza mchezo katika siku iliyopewa heshima yake katika miaka mitatu mfululizo ambayo imefanyika.Hata hivyo ni kama hakuwa na namna dhidi ya Warriors inayoonekana kusheheni mastaa na timu yake kupoteza 127-121.
Hata hivyo kama kawaida yake alionekana kuwapa kejeli wachezaji wa klabu ya Golden State Warriors hasa wale wa benchi katika vipindi tofauti hasa wakati klabu yake ya Raptors ilipokuwa ikiongoza kwa pointi 10.
“Amkuewa akizingumza majungu sana kwa wiki kadhaa sasa, amekuwa akisema kuwa watatufunga kwa sababu pia itakuwa ni usiku wa Drake,” Draymond Green. “Atakuwa ameumia kwa kiasi fulani.”
Stephen Curry alikuwa na pointi 35  huku Kevin Durant akiongeza 30 katika ushindi huo, unakuwa ni ushindi wa tano mfululizo kwa Warriors huku pia ukiwa ni wa tano mfululizo kwao dhidi ya Toronto Raptors.
DeMar DeRozan aliongoza kwa pointi upande wa timu yake, 34 kwa upande wa Raptors, huku Kyle Lowry akiongeza 24 na Toronto wamepoteza mihcezo miwili mfululizo kwa mara ya kwanza mwaka huu. Toronto ilipoteza 121-117 mjini Cleveland dhidi ya Cleveland siku ya alfajiri ya Jumatano.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif