Thursday, November 17, 2016

Uamuzi wa Azam FC kuhusu Kipre Balou


Mchezaji wa Azam FC raia wa Ivory Coast Michael Balou (kulia) akiwa na mkewake (kushoto) wakiwa jukwaani wakifatilia pambano kati ya Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons
Klabu ya Azam FC imethibitisha kwamba, haitoendelea na mchezaji wao Michael Balou ambaye mkataba wake unamalika katika klabu hiyo ya inayoshikilia ubingwa wa AFrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup).
Afisa habari wa Azam Jafar Idd amesema Balou tayari ameshapatiwa barua ya kumtakia kila la heri baadaya ya mkataba wake kumalizika ndani ya Azam  FC.
“Alikuwa ni mchezaji wetu ameitumikia timu kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa mpaka sasa anaondoka mkataba wake umefikia kilele na hayupo kwenye mipango ya mwalimuya baadae kwa maana ya msimu ujao”, amesema Jafar Idd wakati akihojiwa na kituo kimoja cha radio cha Dar es Salaam.
“Taratibu zake na mazungumzo yake na Azam FC vimekwenda vizuri na tayari ameshapewa barua rasmi kumtaarifu hatutakuwanaye kwenye msimu unaokuja.”
Balou alijiunga na Azam mwaka mmoja baada ya ndungu yake Kipre Tchetche kujiunga na klabu hiyo ya Chamazi na anaondoka klabuni hapo miezi michache baada ya ndugu yake kuachana na kjlabu hiyo na kutimkia kwenye falme za Kiarabu.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif